Klabu za Ligi kuu nchini Uingereza zimepiga kura na kuidhinisha soko la kuhama wachezaji lifungwe kabla ya msimu kuanza mwaka ujao.

Mameneja walikuwa wamelalamika kwamba nafasi ya wachezaji kuhama ligi ikiendelea hutatiza klabu na maandalizi.

Kura hiyo haikuwa kwa kauli moja na klabu bado zitaweza kuendelea kuuza wachezaji hadi mwisho wa dirisha la kawaida la kuhama wachezaji.

Dirisha la kuhama wachezaji kote Ulaya huendelea kuwa wazi hadi tarehe 31 Agosti.

Hatua ya klabu hiyo za Ligi ya Premia ina maana kwamba ingawa klabu zitaweza kuendelea kuuza wachezaji hadi siku hiyo, ununuzi utafikia kikomo tarehe 9 Agosti msimu wa 2018-19.

Uhamisho wa wachezaji katika ligi nyingine ndogo za England na Wales (Championship, League One na League Two) hautaathiriwa.

Wasimamizi wa ligi hizo wamedokeza kwamba huenda wakafuata njia hiyo ya Ligi ya Premia lakini wanahitaji mashauriano zaidi.

Klabu za Ligi ya Premia zilizounga mkono mabadiliko hayo bado hazijabainika kabisa, ingawa inaaminikakwamba zilikuwa 14 kati ya 20.

Mabadiliko hayo hata hivyo hayatafupisha muda wa klabu kununua wachezaji kwani soko litafunguliwa mapema na litakuwa wazi muda wa wiki 12, kuambatana na sheria za Fifa.

Agosti, mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane alisema kufungwa kwa soko mapema kutawezesha wachezaji kuangazia klabu zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *