Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz ameeleza jinsi alivyopata msamaha wa matibabu baada ya kuzungumza kwa simu ya video na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.

Ommy ametoa ushuhuda huo katika hafla ya uzinduzi wa albamu yake ya Dedication, albamu ya kwanza kuitoa tangu kaanza muziki miaka kumi iliyopita.

Ommy amesema wakati yupo kwenye matibabu mwaka 2018, Rais huyo mstaafu alikuwa akimfuatilia mara kwa mara hali yake na siku moja alimpigia video call akiwa madaktari ambao walitaka kujua ni nani aliyekuwa akiongea naye na kuhisi kuwa ni baba yake.

“Niliwajibu ndio ni baba yangu lakini ndio Rais wa Tanzania, wakaniuliza wewe ni mtu maarufu huko kwenu?

“Nikawaambia waka-google kunijua zaidi na walipongia kwenye kunitafuta wakaona nyimbo zangu kuanzia pale wakawa wanaambizana wenyewe kwa wenyewe kuwa mimi ni maarufu na wakawa wanaimba baadhi ya nyimbo zangu.

“Kama haitoshi kuna vipimo vya mapafu nilitakiwa kufanyiwa na ilihitajika Euro 25,000 Daktari wa pale aliagiza nisamehewe yote haya yote ni kwa ajili ya wewe baba yangu Jakaya Kikwete,” amesema Ommy.

Kwa upande wake Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, amempongeza ommy kwa hatua ya kuja na albamu hiyo na kukumbushia changamoto za maradhi alizozipitia kuwa hakuna aliyejua kuwa angerudi tena kuimba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *