Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa haruhusiwi kusafiri nje ya nchi bila ya kuwa na kibali cha Serikali.
Diamond aliweka wazi jambo hilo wakati akifanya mahojiano na kipindi cha The Switch kinachorushwa kwenye Wasafi redio.
“Nafikiri ni wasanii wa Wasafi tu unajua sisi haturuhusiwi kusafiri airport bila kibali cha Serikali, mimi nikifika airport nakamatwa siruhusiwi kutoka sijui kwasababu gani lakini nikifika tu pale naambiwa lazima uwe na kibali cha serikali kama unatoka nje ya nchi”. Alisema Diamond.
Diamond kuzuia kutoka nje inaweza kuwa ndio mara ya kwanza unaiskia lakini kila anapotoka kusafiri nje ya nchi anastahili kulipia kibali cha Serikali Sh50,000 ndipo aruhusiwe.
“Basi sifahamu pengine ni taratibu ambazo wana maana, unajua wakubwa bhana wakiweka kitu pengine wanakuwa na maana kubwa ambayo wanakusudia so mimi nachofanya nafuata utaratibu kila naposafiri menejimenti yangu inalipia ili mimi nisafiri ndio maana kuna vitu ukiniambia hatupo rasmi kwenye usajili it does make sense kwangu mimi”. Alisema Diamond.
Lakini hata hivyo msanii huyo hakuweka wazi kibali hicho kinatoka idara gani ya serikali.
Kwa upande wa Baraza Sanaa la Taifa kupitia Kaimu Katibu Mtendaji, Matiko Mniko amesema sheria zipo wazi kwa wasanii wote na wala hakuna sheria ambayo inatungwa kwa ajili ya mtu mmoja.