Kuna mambo mengi yanayoweza kutumika kutoa sifa kwa mastaa wa mambo mbalimbali kisha sifa hizo zikazaa vyeo nakadhalika.
Lakini kwenye Bongo Fleva kuna vitu tofauti sana vinavyomfanyaDiamond Platnumz kuwa STAA wa kweli na LEGENDARY wa muziki.
Kila mmoja miongoni mwa wafuatiliaji wa muziki wa Bongo anafahamu alipotokea Diamond Platnumz na namna alivyohandaika kupata mafanikio.
Lakini kinachozidi kumpa nafasi na heshima kubwa zaidi ni namna anavyoweza kuwasaidia mastaa wengine, chipukizi na mastaa wakubwa kuweza kupata mafanikio kwa kazi zao.
Licha ya kuwaunganisha kwa madirector wakubwa, kufungua milango ya mastaa wa Bongo kufanya kazi nje ya nchi nakadhalika lakini pia Diamond Platnumz amekuwa akitoa elimu kubwa kwa mfumo wa INFORMAL EDUCATION kwa wadau wa muziki hapa Bongo.
Ingawa hana darasa la kufundishia mastaa wengine namna ya kufanikiwa kwenye soko la muziki lakini ni wazi mastaa WANAJIFUNZA.
Na sasa Diamond Platnumz ametoa funzo la namna ya kukubali kulipwa na makampuni makubwa ya Marekani na Ulaya ya kusambaza kazi za wasanii.
Unajua Diamond Platnumz analipwa kiasi gani na kampuni ya Vevo? Ili kampuni hiyo kuweza kufanikiwa kupata saini ya Diamond Platnumz kwenye mikataba yao iliwalazimu kukubali kumlipa sawa na mastaa wengine wa Marekani na hilo ndio somo ambalo Diamond Platnumz amelitoa kwa mastaa wa Bongo, USIKUBALI kuwepo kokote pale kwenye faida ya kibiashara ‘kama staa’ BILA KUTENGENEZA MKWANJA UNAOSTAHIKI.
Kuna siku niliulizwa kwanini we haupo Vevo… Nikawambia: “uwepo wa msanii @VEVO anatakiwa msanii alipwe zaidi ya alivyokuwa analipwa kwenye Youtube channel ya kawaida.. Vevo wenyewe pia wamtambue kuwa kuna msanii anaitwa Nasibu Abdul aka Diamond toka Tandale, na pia anacholipwa msanii wa Marekani kwa view moja ama tangazo lolote liekwalo mwanzo ama lipitalo katikati pindi ya utazamaji wa video hyo basi nae anapaswa kulipwa hivyohivyo…na mbali tu ya kumlipa VEVO yapaswa kwa namna moja au nyingine kusaidia kupromote maana ni biashara yao wote na kila msanii ana shabiki zake na ukubwa na nafasi yake atokapo”…..hivyo nikawambia: “siku mkiniona nipo vevo basi jua nimeyakamilisha haya, vinginevyo wacha niendee kuokota senti mbili tatu, kwenye chanel yangu ya Youtube kawaida….
SABABU YA KUYASEMA HAYA:
Ni kutaka kuwafahamisha ama kuwaamsha baadhi ya wasanii wenzangu watambue kuwa Mziki wetu hata kama hauko mkubwa saaaana ulimwenguni, ila Mwenyez Mungu kausaidia kuufikisha sehem flani, hivo wasanii lazma tujitambue na Tuwe na Misimamo na kazi zetu, vilevike umakini kwenye maamuzi ama hatua yoyote tutayoichkua juu ya sanaa zetu kwa sasa, maana tuliamualo leo linaweza kutujenga ama kutubomoa baadae… nafaham wasanii wengi hawakuwa wakilifaham hilo na badala yake kuingia @VEVO kupitia watu kati ama madalali na kuambulia status mtaani kuwa wako @VEVO ilhali nyuma kuna watu wanawadhuLumu mamilioni ya pesa zitokanazo na jasho lao…” kwa uchungu wa kufaham namna gani inauma msanii ukinyonywa kazi yake ndio umenifanya nilizungumze hili leo, ila ukiona kwa namna moja au nyingine nimekosea Tafadhali mnisamehe… -SIMBA #MALENGO