Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz jana amefanya show ya kufa mtu jijini Nairobi nchini Kenya.
Diamond aliwapagawisha mashabiki waliofika kushuhudia show hiyo kwani walipata burudani ya kutosha kutoka kwa mwanamuziki huyo pamoja na timu yake nzima ya WCB ambapo waligusa nyoyo za mashabiki.
Katika show hiyo iliyojulikana kama Safaricom Private Party, Diamond alipiga nyimbo zake mbali mbali zilizotamba masikioni mwa watu.
Warembo kutoka jijni humo walionekana kuguswa zaidi muimbaji huyo kutoka WCB kitu ambacho kilileta burudani ya aina yake kwa waliohudhuria.
Diamond anatarajia kuzindua albam yake mpya inayokwenda kwa jina la A Boy From Tandale itakayotoka mwezi.