Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameweka wazi kiasi cha kodi anacholipa kwa mwaka ambapo ni Tsh Bilioni 1.7 kila mwaka.

Diamond ameeleza hilo kwenye mkutano wa Zoom ambao umekutanisha wadau wa siasa na viongozi mbali mbali kuelekea miaka 60 ya Uhuru.

“Serikali imetengeneza mazingira rafiki kurasimisha tasnia ya muziki na kuiwekea wepesi kwenda kwenye sekta rasmi, mfano mimi kutoka kwenye uwanamuziki mpaka nimekuwa mkurugenzi wa makampuni mbalimbali”

“Nilikuwa nafanya mahesabu hapa namna ya kimapato huu mwaka kwa kodi ambazo tumezichangia ni Bilioni 1.7, najivunia Serikali imeniwekea mifumo sahihi najiona ni mlipa kodi na nachangia kwa namna moja au nyingine”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *