Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz ameingia kwenye mkataba wa kuwa Balozi wa Mtandao wa Mawasiliano nchini Airtel.

Diamond atakuwa na kazi ya kutangaza ubora na uimara wa huduma ya Airtel hasa matumizi ya Intaneti ya mtandao huo.

Kwa takribani siku kadhaa nyota huyo aliwaweka roho juu mashabiki wake baada ya kuwaambia kuwa atakuwa tayari kumtambulisha mpenzi wake mpya.

Diamond alizua shauku kubwa kwa mashabiki hao kwenye moitandao ya kijamii kwa kutaka kujua ni mpenzi gani atakayetambulishwa na Diamond Platinumz.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *