Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kwa amekuwa mwanamuziki wa kwanza kusini mwa jangwa la sahara kupata watazamaji milioni tano katika mtandao wa Youtube, kupitia chaneli yake ya youtube.
Kwa karibu anafuatwa na Davido akiwa na watazamaji milioni 2.38, Burna Boy milioni 1.82 na Wizkid milioni 1.68.
Mafanikio haya ya sasa ya Diamond yanakuja yakifuata rekodi aliyoiweka mwaka jana (2020) baada ya wimbo wake maarufu ‘Waah’ aliomshirikisha mwanamuziki wa Koffi Olomide wa DRC kutazamwa na watu milioni 8 ndani ya saa chache baada ya kibao hicho kutoka, na kuvunja rekodi iliyowekwa na mwanamuziki wa Nigeria Davido baada ya kibao chake ‘Fem’ kuwavuta watazamaji milioni moja ndani ya saa 9 tangu kibao hicho kilipoachiwa.
Rekodi nyingine iliyowekwa na mwimbaji huyo ni kuwa msanii wa kwanza kusini mwa jangwa la Sahara kuwa na watazamaji bilioni moja youtube.
Katika kipindi cha miaka 10 iliopita, mwanamuziki huyo alieshinda mataji kadhaa amekuza muziki wa bongo fleva kuwa maarufu – muziki wa kipekee wa Tanzania unaotoa nyimbo za kimapenzi zilizochanganywa na midundo ya kisasa inayotokana na muziki wa jadi wa taarab kutoka pwani ya Afrika.
Diamond Platinumz ni mwanamuziki alie na bidii na maonyesho yake huvutia mashabiki wengi, kulingana na DJ Edu, ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha runinga cha kila wiki cha muziki wa Afrika cha BBC.
Huku akiwa na asilimia 43 ya mashabiki miongoni mwa raia milioni 55 nchini Tanzania wanaoweza kuingia katika mtandao, kupitia simu aina ya smartphones, kuna mashabiki