Wanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Nandy jana wamehudhuria kikao cha Bunge kusikiliza bajeti ya wizara ya habari, Sanaa, Utamuduni na Michezo.
Wanamuziki hao walitambulisha Bungeni na mwenyekiti wa Bunge, Musa Azzan baada ya kuwasili Bungeni hapo.
Mbali ya Diamond na Nandy wengine waliotambuliwa ni mwanamuziki Mrisho Mpoto na msanii wa filamu Monalisa.
Zungu amesema wote ni wageni wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo. Bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19 inasomwa leo.