Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameahidi kulipia BIMA ya Afya kwa watoto 300, kutoa mitaji kwa akina mama 200, kutoa Boda boda 20 na kukarabati Shule zote za msingi zilizopo ndani ya Kata aliyozaliwa ya Tandale.

Mwanamuziki huyo amesema hayo wakati wa sherehe fupi ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika Oktoba 2 mwaka huu katika ofisi za wasafi Tv jijini Dar es Salaam.

Diamond amesema kuwa kesho Tarehe 5 Oktoba 2018 atatimiza ahadi hiyo ikiwa na pamoja kuchinja ng’ombe na kusherehekea na watu wake wa Tandale.

Pi amesema kuwa msaada huo utaenda moja kwa moja kwa wamama na watoto hao wa Tandale bila kupendelea mtu yoyote hivyo amewaomba wajitokeze kwa wingi.

Katika siku yake kuzaliwa mwanamuziki huyo alitumia nafasi hiyo kuonesha mjengo wake mpya ambao ndiyo yatakuwa makazi yake mapya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *