Mkali wa Bongo fleva kutokea WCB, Diamond Platnumz anatarajia kutumbuiza kwenye utoaji wa tuzo ya mwanasoka bora Afrika kesho kutwa zitakazofanyika jijini Abuja nchini Nigeria.
Diamond Platnumz ataungana na wanamuziki kutoka nchi mbali mbali za Afrika akiwemo Mr Flavour na Yemi Alade kutoka Nigeria, Muffinz kutoka Afrika Kusini pamoja Dj Jimmy nae atakuwepo kutoa burudani siku hiyo.
Tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika hutolewa kila mwaka barani Afrika kwa mchezaji aliofanya vuzuri katika klabu pamoja na timu ya Taifa mpaka kupelekea kushinda tuzo hiyo kubwa katika upande wa soka Afrika.
Wachezaji kibao waliteuliwa kuwania tuzo hiyo ambapo wamechujwa mpaka kufikia 3 bora ambao ni Pierre Emerick Aubemayang kutoka klabu ya Borrusia Dortmund na timu ya taifa ya Gabon, Saido Mane kutoka klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Senegal pamoja na Riyad Mahrez kutoka klabu ya Leicester City na timu ya taifa ya Argelia.
Utoaji wa tuzo hiyo utafanyika siku ya Alhamisi tarehe 5 Januari mwaka huu katika jiji la Abuja nchini Nigeria.
Mbali na Diamond Platnumz kutumbuiza kwenye utoaji wa tuzo hiyo pia anatarajia kutumbuiza kwenye ufunguzi wa kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika nchini Gabon Januari 14 mwaka huu.