Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametangaza collabo yake ya kimataifa na Mwanamuziki wa Marekani, Rihanna ambayo amesema itapatikana kwenye album yake.
Akiwa Nchini Uingereza katika kuendelea kuitangaza EP yake mpya ya #FOA (First Of All), Star huyo amefanya Listening Party nchini humo ambapo Diamond Platnumz alizungunzia collabo hiyo.
“Ningependa Kufanya Kazi na Rihanna, Nahisi Itakuwa Ni Ngoma Kali Sana, Kama Sio Kwenye Album Hii Basi Album Yangu Inayofuata.
Diamond amesema kuwa ameshaongea na Rihanna na Timu Yake Na Kila Kitu Kipo Sawa, Kwa Mambo Yanayoendelea Kwa #Rihanna Sasa, Inaweza Ikafanya akawepo Kwenye Album Hii Au Ijayo”.