Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametangaza ziara yake ya muziki nchini Marekani ambapo anatarajia kutumbuiza jumla ya majiji 12 nchini humo.
Diamond amesema kuwa ziara hiyo itarajia kuanza Juni 22 hadi Julai 23 mwaka huu ambapo atatoa burudani katika majiji makubwa nchini humo ikiwa ni kwa ajili ya kuitangaza albamu yake mpya itakayotoka mwezi Machi.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Diamond amewatangazia mashabiki wake wa Marekani kuwa atatoa burudani kwa ajili ya kuitambulisha albamu yake mpya ‘A Boy From Tandale’.
Majiji ambayo Diamond anayotarajia kufanya shoo ni New York, Los Angeles, Minnesota, Houston, Seattle, Kansas City, Washington DC, Boston, Atlanta, Columbus, Philadephia, Dallas.
Diamond anatarajia kuachi albamu yake mpya ‘A Boy From Tandale’ ifikapo mwezi machi mwaka huu ikijumuisha nyimbo zake zote.