Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza ameonesha jumba lake la kifahari lililopo nchini Afrika Kusini.
Diamond alionesha jumba hilo kubwa la kifahari lililopo jijini Johannesburg nchini humo hivyo mwanamuziki huyo anakuwa mwanamuziki wa kwanza kutoka Tanzania kumiliki jumba la kifahari.
Mbali na kuwa na vyumba vingi na samani za kupendeza, nyumba hiyo pia ina bwawa la kuogelea ndani yake. “Ni vizuri sana kurudi nyumbani!” Alisema Diamond chini ya video iliyoonesha jumba hilo.
Katika video hiyo, baadhi ya washiriki wa timu yake ya muziki walionekana wakistarehe ndani ya jumba hilo katika vyumba tofauti vya kulala.
Diamond alitumia fursa hiyo kutangaza kuwa baada ya kupumzika nchini Afrika Kusini kwa muda wataendelea na ziara yao ya muziki katika mataifa mbalimbali.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na ripoti kuwa Diamond mwenye umri wa miaka 32 anamiliki jumba la kifahari nchini Afrika Kusini.