Mwanamuziki nyota wa pop nchini, Diamond Platnamuz amemjibu msanii mwenzake aliyekuwa Harmonize kuhusu tuhuma za unyonyaji na njama za kushusha wengine, lakini akahimiza jitihada na kujiamini ili Watanzania waliteke soko la kimataifa.

Diamond alikuwa akizungumza katika kipindi cha The Switch cha Wasafi FM jana jioni baada ya kuachia albamu yake ya kidigitali au EP.

Katika kipindi hicho, watangazaji walimuuliza nyota huyo wa miondoko ya Bongo Fleva kuhusu tuhuma alizotoa Harmonize, ambaye alidai kuna njama za lebo hiyo kuwashusha wasanii wanaoanza kuwika, maneno aliyosema mara tu alipotua nchini akitokea Marekani mwaka jana.

Bosi huyo wa Konde Music WorldWide pia alisema mikataba mingi ya Wasafi na wasanii ni ya kinyonyaji.

Kuthibitisha hoja zake, Harmonize aliwasikilizisha waandishi wa habari mazungumzo yake na sauti aliyodai ni ya Rayvanny kuonyesha jinsi asivyoridhishwa na mambo ya Wasafi, jambo lililoibua ubashiri kuwa nyota huyo wa “Kwetu” pia yuko mbioni kujiengua

Alisema milango mingi ipo wazi, ila kinachotakiwa ni kujituma na ubunifu, akitoa mfano wa wimbo wa “Sukari” wa Zuchu, ambao alisema umevunja rekodi aliyokuwa anaishikilia ya kuwa na namba kubwa katika YouTube kuliko kazi ya Mtanzania yoyote kwa sasa.

Kwa sasa Diamond, ambaye alichomoza kimataifa na video ya “Number One aliyoshirikiana na Mnigeria Dovido, anaitangaza albamu yake ya kidigitali aliyoipa jina la FOA, ikimaanisha awali ya yote (First of All).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *