Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amefunguka na kusema kuwa katika safari yake ya mapenzi hakuna mwanamke aliyemliza kama Wema Sepetu wakati walipokuwa kwenye mahusiano.
Diamond amesema kuwa alipata wakati mgumu sana wakati yupo kwenye mahusiano na Wema Sepetu kwasababu wakati huo Wema alikuwa staa zaidi yake na yeye alimpenda sana hivyo kukampelekea matatizo ndani ya familia yake.
Mwanamuziki huyo ameendelea kwa kusema kuwa Wema Sepetu alisababisha mpaka Diamond agombane na familia yake kutokana na vitendo vya staa huyo wa Bongo Movie.
Diamond amekiri kuwa kwa kusema kuwa hakuna mwanamke ambaye aliyemliza kwenye mapenzi kama Wema Sepetu hadi sasa alipofikia.
Pia mwanamuziki huyo amekiri kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Zari huku akibainisha kuwa hiyo siyo kiki bali ni ukweli mtupu.