Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema amefurahi kufanya kazi na Barnaba msanii ambaye amemfanya kuingia kwenye tasnia ya muziki huo.

Diamond amefunguka hayo kwenye uzinduzi wa albam ya Loves Sounds Different yenye nyimbo 18, nyimbo zilizobeba jumla miaka ambayo Barnaba amedumu ndani ya sanaa hiyo.

Diamond na Barnaba wameshirikiana kwa maara ya kwanza katika albam hiyo mpya ambayo imeanza kufanya vizuri katika platform mbali mbali za muziki nchini.

Diamond alisema Barnaba ndiye msanii aliyemfanya kuingia kwenye tasnia ya muziki huo kutokana na namna anavyojua kuandika mashairi ikiwa ni sambamba na kuwa na sauti nzuri ya kumsahawishi msikilizaji kusikiliza kazi zake.

“Barnaba ni msanii mkubwa nimejifunza muziki kupitia kazi zake nimekuwa shabiki yake wa muda mrefu nafurahi kufanya naye kazi ya pamoja, ni moja ya ndoto zangu kutokana na kuwa moja ya wasanii waliokuwa wananivutia tangu nikiwa na ndoto ya kuimba,” alisema.

Licha ya kufanya kazi na Diamond Platnumz kwenye albam hiyo Barnaba amefanya kazi na Alikiba ambaye ni mpinzani wa Diamond kwenye muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *