Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema haoni tatizo kuchukua asilimia 60 ya mapato ya msanii wake.
Amesema anafanya hivyo kwani mziki ni biashara inayohitaji uwekezaji mkubwa na mpaka msanii awe mkubwa inatumika kati ya Sh 400-500 milioni zinakuwa zimetumika kuwekeza kwa wasanii.
“Mziki ni biashara, unaona sisi tunavyochukua vijana walikuwepo katika malebo flani ila hawakuwa wakubwa.
Amesema kuwa “Ila wanapokuja kwetu sisi wanajua kuimba tunachukua kile anachofanya kuwa biashara kiweze kuingiza hela, ndio maana wasanii wa Wasafi wanakuwa wakubwa na matajiri,”.
“Biashara inapokuwa kubwa wengi wa vijana wanataka ile biashara aichukue yeye peke yake wakati ni uwekezaji nilifanya haya kwa kuwekeza mamilioni ya pesa zangu ndani yake,” amesema
Diamond amesema lakini sasa msanii anaposema wanataka kuondoka na biashara nzima siwezi kuruhusu hilo, napaswa kurejeshewa pesa zangu na faida pia.