Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amefikishwa Polisi jana kuhojiwa kutokana na kusambaza video zake zisizo na maadili katika mitandao ya kijamii.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa Bungeni wakati akijibu swali juu ya kanuni za maudhi ya Mitandaoni.

Juzi usiku zilisambaa video zikimuonesha Diamond akiwa na wanawake wawili tofauti wakiwa nusu utupu na kuleta taharuki kwa mashabiki wake.

Pia Dkt. Mwakyembe amesema Msanii Faustina Charles (Nandy) naye atahojiwa na Polisi kufuatia video yake ya faragha akiwa na Msanii mwenzake Billnass kusambaa mitandaoni.

Mwakyembe ametoa wito kwa vijana kuwa mitandao si kokoro la kupeleka uchafu wote ambao umezuiwa na sheria na kwamba nchi ina utamaduni wake ambapo inahitajika kulinda kizazi cha sasa na cha kesho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *