Mastaa waliotesa Uingereza na kisha kutorokea Ufaransa, Dimitri Payet na Memphis Depay wameanza kuzifungia mabao timu zao mpya.
Mshambuliaji wa zamani wa West Ham United, Payet alifunga mkwaju wa faulo na kuiwezesha timu yake ya Marseille kuitandika Guingpan 2-0.
Wakati Payet aking’aa na Marseille, mshambuliaji wa zamani wa Man United, Memphis Depay nae aliingia kipindi cha pili kwenye mchezo wa Lyon na Nancy na kufunga bao moja kwenye ushindi wa 4-0.
Mbali ya kufunga bao hilo pia Depay alipelekea timu yake kupata penati iliyozaa bao la tatu baada ya kuchezewa vibaya kwenye eneo la hatari.