Mchezaji wa Barcelona, Ousmane Dembélé anatajia kurejea uwanjani hivi karibuni baada ya kupona mejeraha yaliyomuweka nje kwa miezi mitatu.
Mtandao wa klabu hiyo umethibitisha hilo baada ya mchezaji huyo kuonekana kupona majeraha yake ya mguu wa kushoto aliyoyapata wakati wa mchezo wao dhidi ya Getafe Septemba 16 mwaka jana.
Taarifa ya mtandao huo umesema kuwa “Kurudi kwa Ousmane Dembélé uwanjani kunakaribia. Kwa kweli, Jumanne hii alipata matibabu kutoka kwa Huduma za Kliniki za Klabu na, kwa hiyo, Ernesto Valverde anaweza kumtumia. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 atakuwa na uwezo wa kucheza tena, miezi mitatu na nusu baada ya kupasuka kwa tendon ya biceps ya mguu wake wa kushoto, majeruhi yaliyotokea dhidi ya Getafe mnamo Septemba 16,”.
Pia uliongeza kwa kuandika kuwa “Licha ya haja ya kufanyiwa operesheni nchini Finland, Dembélé haraka alianza mchakato wake wa kurejesha na kuanza kufanya kazi yake Ciutat Esportiva mnamo Disemba 6, kumalizika Januari 2. Kabla ya kuumia, alicheza dhidi ya Espanyol na Juventus katika michezo yake ya kwanza akiwa na Barcelona, assist yake ya kwanza ilikuwa kwa Suárez,”.
Dembélé alisajiliwa na Barca msimu huu akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa dau la paundi milioni 105 usajili uliopita.