Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI), Robert Boaz, ametoa onyo kali kwa watumiaji wa mitandao ya jamii kwa lengo la upotoshaji na kuliagiza Jeshi la polisi kuanza mara moja kuwashughuliakia na kuwachukulia hatua za kisheria watu wenye tabia hiyo.

Hayo yamezungumzwa na mkurugenzi huyo mara baada ya mitandao ya kijamii kusambaza video yenye habari inayonyesha uwepo wa mchele wa plastiki nchini.

Boaz amekanusha uwepo wa mchele huo wa plastiki na kumsaka mtu aliyerekodi video hiyo ili asaidie kutoa taarifa zaidi.

Pia amewaomba wananchi kutumia vizuri mitandao ya kijamii na kujiepusha kusambaza taarifa zisizokuwa na ukweli, kwani ni hatari na husababisha madhara makubwa katika jamii.

Aidha waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia na wazee na watoto , Ummy Mwalimu ametaarifiwa na  Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA), kuwa hakuna mchele wa aina hiyo nchini.

Waziri Ummy amewasisitizia watanzania kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii, na kuepuka upotoshaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *