Mkuu wa wilaya ya Pangani, Zainab Abdallah amefunguka na kudai anawaheshimu wanawake wenzake wanaojishughulisha kutafuta pesa kwa namna moja ama nyingine huku akiwataka wasiwape upenyo baadhi ya watu ambao wanataka kuwarudisha nyuma kimaendeleo.

Bi. Zainab ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii asubuhi ya leo baada ya kuwepo kwa imani potovu kwa baadhi ya wanaume ambao wanawakatazia wanawake zao kutojihusisha na ufanyaji kazi wa aina yeyote ile.

 “Heshima ya mwanamke ni kujishughulisha na kuingiza kipato chako mwenyewe, haijalishi umeajiriwa au kujiajiri. Haijalishi unauza Mama Ntilie, unajishughulisha na kilimo au biashara yoyote ile. Kikubwa heshimu unacho kifanya na usimpe nafasi mtu kudharau kinacho kuingizia rizki. Nawapa heshima wanawake wote ambao wanajishughulisha na wanajua uchungu wa kutafuta pesa, nawapenda”,.

Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah amesema hayo ikiwa kama ni ishara ya kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo huwa inaadhimishwa kila ifikapo Marchi 8 ya kila mwaka na kudai ataendelea kufanya hivyo mpaka kufika tarehe hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *