Mkuu wa Wilaya ya Serngeti mkoani Mara, Nurdin Babu amesema kuwa wilaya hiyo inahitaji zaidi ya tani 4.1 za chakula ili kunusuru maisha ya kaya zaidi ya 32,000 kutokana na mahindi yao kukauka kutokana na ukame uliupo sasa.
Mkuu wa wilaya huyo amesema kuwa hali ya chakula kwa mwaka huu sio ya kuridhisha kutokana na mvua vuli kutonyesha kwa wakati.
Babu ameongeza kwa kusema wapo baadhi ya watu, wanakula mlo mmoja na wengine mitatu kwa siku na hakuna mtu wala mifugo iliyokufa kutokana na ukame, kwa sasa bei ya mahindi debe moja linauzwa Sh 15,000 ambapo upatikanaji wa chakula kwenye masoko wa kiwango kinachohitajika.
Kutokana na hali hiyo ya ukame mkuu wa wilaya huyo amewataka wananchi kuhifadhi chakula kilichopatikana na kuacha utamaduni wa kutumia nafaka kutengenezea pombe za kienyeji na kila familia iwe na ghala la kuhifadhi chakula.
Pia amesema mbali na ukame, mvua kutonyesha kutokana na mabadiliko ya tabianchi pia yapo malalamiko ya wananchi kuhusu tembo kuvamia mashamba yao na kula mazao yote na kueleza kuwa changamoto hiyo serikali inalifahamu na takwimu za uharibifu zilikwisha wasilishwa wizara ya maliasili na utalii ili kuli pa kifuta machozi kwa wote walioathirika.