Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amemuagiza Ofisa Mipango Miji wa Manispaa hiyo kuhakiki majina ya wakazi wa eneo la Jangwani ili kubaini waliopewa viwanja Mabwepande na kuamua kupangisha wengine.
Pia Mjema amesema Manispaa hiyo itawachukulia hatua wakazi wote wa Jangwani waliopewa viwanja Mwabepande lakini wameamua kuwachukuwa wapangaji na kuwaweka katika nyumba zao zilizopo eneo hilo huku wakijua kuwa nyumba hizo sio mali yao.
Mjema aliyasema hayo wakati aliotembelea eneo la Jangwani ili kuona hali halisi baada ya mvua iliyonyesha jijini Dar es Salaam juzi na kusababisha kifo cha mtu mmoja katika eneo hilo.
Alisema kuna wananchi waliopatiwa viwanja maeneo ya Mamwepande na kutakiwa kuondoka katika eneo hilo ambalo ni hatari, lakini wakaamua kutafuta watu na kuwakodisha kuendelea kuishi katika nyumba zao zilizopo katika eneo la Jangwani.
Mjema pia amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo ya mabondeni katika wilaya hiyo kuondoka katika maeneo hayo kwa kuwa ni hatari hasa kwa kipindi hiki cha mvua za masika.