Kuna msemo unaosemao ‘lisemwalo lipo kama halipo laja’ msemo huo unamgusa mkali wa rap nchini Darassa baada ya kutuhumiwa kutumia madawa ya kulevya.
Baadhi ya watu nchini wamekuwa wakimtuhumu mwanamuziki huyo kuwa anatumia madawa ya kulevya kutokana na ukimya wake kwenye muziki wa Bongo Fleva.
Kwa upande wa mwanamuziki huyo amekanusha kutumia dawa za kulevya kwani watu wasiopenda maendeleo yake ndiyo wanaosambaza habari hizo mbaya kwa jamii.
Darassa amesema kuwa hakuna kitu kama hicho ila ni maneno ambayo yanavumishwa kutokana na ukubwa wa jina lake lakini haonekani katika mitandao na katika maeneo ya starehe.
Darassa ameongeza kuwa watu wanaogopa vitu vyenye ukimya wakijua mshindo wake huwa ni mkubwa hivyo wanazusha mambo kama hayo.