Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amepokea taarifa ya maendeleo ya mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika gesi asili (LNG Plant) kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Likong’o, Mchinga mkoani Lindi.

Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Statoil ya nchini Norway ambayo ni moja ya kampuni zitakazowekeza katika mradi huo Oystein Michelsen alimueleza Rais Magufuli kuwa ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani bilioni 30 sawa na zaidi ya Sh trilioni 65 za Tanzania na kwamba uzalishaji unatarajiwa kuchukua muda wa zaidi ya miaka 40 baada ya kuanza.

Rais Magufuli: Akiwa  na baadhi ya wawakilishi kutoka nchini Norway ambao wamemkabidhi taarifa ya ujenzi wa kiwanda cha gesi nchini.
Rais Magufuli: Akiwa na baadhi ya wawakilishi kutoka nchini Norway ambao wamemkabidhi taarifa ya ujenzi wa kiwanda cha gesi nchini.

Mwakilishi huyo alibainisha kwa kusema kuwa Serikali ya Norway ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa manufaa ya pande zote na ameomba Serikali ya Tanzania iendelee kutoa ushirikiano ili kufanikisha ujenzi wa kiwanda hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *