Mkoa wa Dar es Salaam umeongoza kwa lugha ya matusi mtandaoni licha ya kuwepo kwa sheria ya makosa ya mtandao.

Takwimu hizo zimetolewa na jeshi la Polisi nchini baada ya uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo katika mikoa hapa nchini.

Pia Mkoa wa Mwanza nao umebainika kuwa kinara kwa upande wa  makosa ya wizi wa fedha mtandaoni ukilinganisha na mikoa mingine.

Takwimu zilizotolewa na jeshi la polisi zimeonyesha kuwa jumla ya matukio 327 ya matusi mtandaoni  yameripotiwa kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu.

Msemaji wa jeshi hilo, ACP Barnaba Mwakalukwa amesema matukio mengi ya makosa ya  matusi yanatokea wilaya ya Temeke.

Hata hivyo, Mwakalukwa amesema takwimu hizo zinaonyesha kupungua ikilinganishwa na mwaka jana ambapo matukio kama hayo 911 yaliripotiwa na wilaya ya Kinondoni iliongoza.

Amesema jumla ya watuhumiwa 315 walikamatwa kuhusiana na makosa ya uhalifu mtandaoni na kesi 153 zimefikishwa mahakamani. Kati ya kesi hizo wahusika katika kesi 19 walikutwa na hatia na nyingine zipo chini ya upelelezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *