Mashindano ya kuonyesha vipaji vya kucheza maarufu kama DANCE 100% yamezinduliwa rasmi hii leo jijini Dar es Salaam.
Waratibu wa shindano hilo, East Africa TV wamesema kuwa mwaka huu mashindano hayo yatadhaminiwa na kampuni za Vodacom na Coca-Cola.
Mchujo rasmi wa mashindano hayo unatarajiwa kuanza kufanyika kwenye viwanja vya leaders kwa kufanyika mchujo awali tarehe 16 hadi tarehe 30 mwezi huu.
Makundi ya ku-dance yamehimizwa kujitokeza kuonyesha vipaji na kushindana huku wananchi wakiombwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchuano wa makundi hayo na hakutakuwa na kiingilio.
Mashindano haya yatakuwa yakirushwa na kituo cha Televisheni cha East Africa na kundi litakaloshinda litapata zawadi ya fedha taslim shilingi milioni 7 huku mshindi wa pili akipata milioni 2 na kundi litakaloshika nafasi ya tatu likipata milioni 1.