Mkazi  wa  jiji la Dar es Salaam, Abdallah Juma aliyewahi kukamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akidaiwa kujifanya daktari amenaswa tena katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa kufanya kazi katika hospitali hiyo wakati sifa za udaktari hana.

Juma alinaswa jana ndani ya Hospitali ya Amana, majira ya mchana, akijifanya daktari, baada ya kuwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo.

Kukamatwa kwa Juma  kunakuja ikiwa ni miezi mitatu tu imepita tokea Juni 19 mwaka huu alipo kamatwa katika hospitali ya Muhimbili kwa kujifanya daktari.

Katika hospitali ya Muhimbili kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika maabara kuu  huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma aliyokuwa akiitoa kitu ambacho kilisababisha kushtukiwa na kukamatwa.

Baada ya kukamatwa Uongozi wa hospitali hiyo ulifanya uchunguzi na kubaini kuwa kijana huyo hakuwa daktari bali daktari feki kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa mara baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo. Daktari wa Kitengo cha Watu wanaoishi na Virusi  vya Ukimwi (WAVIU),    Shani Mwaruka alikiri kukamatwa kwa  kwa mtuhumiwa huyo.

Alisema, Juma alinaswa baada ya uongozi kupata malalamiko kutoka kwa  watu waliokuwa wakihitaji huduma  katika hospitalini hiyo.

Alisema tayari hospitali hiyo iliweka mtego imara wa maofisa wake, ambapo Juma aliingia bila hofu yeyote na kukutana na watu ambao alitaka wampe fedha ili awahudumie ndipo aliponaswa.

Baadhi ya watu waliodaiwa kuombwa fedha na  daktari huyo feki, wamesema aliahidi kuwatafutia kazi mbalimbali katika hospitali hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *