Mtu mmoja, Abdalah Juma amekamatwa akijifanya daktari katika hospitali ya Taifa ya Muihimbili.

kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika maabara kuu ya Hospitali hiyo huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma aliyokuwa akiitoa kitu ambacho kilisababisha kushtukiwa na kukamatwa.

Baada ya kukamatwa Uongozi wa hospitali hiyo ulifanya uchunguzi na kubaini kuwa kijana huyo hakuwa daktari bali daktari feki kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa mara baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeweka mikakati mbalimbali ya kupambana na wahalifu wakiwamo watu wanaojiita ni madaktari kama huyo ambaye alikamatwa  jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *