Chama Cha Wananchi (CUF) kimekiri kuwa mtu aliyekatwa kisigino kwenye vurugu zilizotokea siku ya jumamosi ni mlinzi wa chama hicho.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa Habari wa chama hicho, Abdul Kambaya huku akisema mlinzi huyo na wenzake walikwenda Mabibo kwa ajili ya kufanya doria maeneo hayo yaliyokuwa yanafanyika mkutano.

Kambaya amesema kuwa mlinzi huyo amekatwa mapanga na watu wanaomuunga mkono, Maalim Seif baada ya kuvamia mkutano uliofanyika maeneo ya Mabibo jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

Ameongeza kwa kusema kuwa si kweli mlinzi huyo alipigwa na wananchi wenye hasira kali bali alipigwa na wafuasi wa CUF wanaomuunga mkono katibu mkuu, Maali Seif Sharif Hamad.

Pia ametumia nafasi hiyo kuomba radhi waandishi wa habari ambao waliumizwa kwenye vurugu hizo japokuwa hazijafanywa na wao.

Siku ya Jumamosi waandishi wa habari walipata kipigo kutoka wafuasi wa CUF wanaomtii, Profesa Lipumba baada ya kuvamia mkutano wa CUF wanaomtii Maalim Seif.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *