Klabu ya Crystal Palace jana imeifunga Arsenal 3-0 kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza iliyochezwa katika uwanja wa Selhurst Park.
Palace walianza kuongoza kupitia kwa Andros Townsend kisha dakika chache baadaye Yohan Cabaye akapachika goli la pili.
Luka Milivojevic akaiandikia Palace goli la tatu kwa mkwaju wa penalti na kuifanya kuwa alama sita juu ya mstari wa kushuka daraja.
Katika kipindi cha pili Arsenal hawakuweza kupiga shuti lililolenga lango la Palace na tokea ajiunge na Arsenal mwaka 1996, Wenger hajawahi kumaliza nje ya nne bora
Baadhi ya mashabiki wa Arsenal waliosafiri kutoka London walibeba mabango yanayomtaka mfaransa huyo kuachia ngazi.
Arsenal ipo alama saba nyuma ya timu ya nne ambayo ni Manchester City ikiwa pia imesalia na michezo nane kabla ya ligi kumalizika.
Iwapo Arsenal itashindwa kuingia nafasi nne bora, itakuwa ni mara ya kwanza tokea imeanza kunolewa na Arsene Wenger mwaka 1996.