Mwanamuziki wa Bongo Fleva, CPwaa amefunguka kuachia kolabo yake mpya na marehemu Albert Mangwair ambayo pia Chege amehusika kwenye ngoma hiyo.

CPwaa amesema ngoma hii imetumia verse ya Ngwair ambayo aliiandika miaka 10 iliyopita, na iliondolewa kwenye “Action” mkwaju uliowakutanisha pamoja na Ms. Triniti na Dully Sykes.

Verse ya Ngwair ilibidi iondolewe na afanye hook tu kwa sababu CPWAA alitaka kumuingiza Ms. Triniti na ngoma tayari ilikuwa imejaa, Ngwair alikubali ombi hilo na ‘Action’ ikafanyika.

Ngoma mpya ya Pwaa ‘FIRE’ imetoka ikiwa na ile verse ya Ngwair iliyochinjwa. Pia ameweka wazi kuwa asilimia 20 ya mapato ya wimbo huu yatakwenda kwenye familia ya marehemu Ngwair na tayari wamesaini mikataba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *