Mwanamuziki wa hip hop Bongo, Country Boy na Dipper Rato wana jambo lao kwani wanatarajia kuachia ngoma ya Pamoja baada ya kuthibitisha hilo.

Country Boy weekend hii walikuwa pamoja kwenye tukio la Marioo ambapo wote kwa pamoja walifunguka kuhusu ukaribu wao.

Wawili hao kila mmoja anafanya muziki nzuri hali ambayo imeleta shauku zaidi wawili wakiachia kazi ya Pamoja hivyo mashabiki wakae tayari kwa kuwaokoa.

Kila mmoja alikiri lolote linaweza kutokea huku wakiwataka mashabiki kukaa mkao wa kula kwani wanatarajia kuachia ngoma ya Pamoja ya wawili hao baada ya kimya cha muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *