Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Country Boy amesema anatarajia kutoa albam yake mpya aliyowashirikisha wanamuziki wa kimataifa.

Country Boy amesema kuwa albam yake hiyo inayosimamiwa utayarishaji wa mwisho na Harmy B itaingia mtaani mapema mwakani ikiwa na collabo kubwa ikimjumuisha pia Patoranking kutoka Nigeria.

Country amesema kuwa “Albam yangu nzima mastering itasimamiwa na Harmy B. Ujue yule Hermy ni kama bro (kaka) anapenda muziki wangu lakini kuna makubaliano tumeyafanya ili kukamilisha, ujue ile ni kazi yake,”.

Pia ameongeza kuwa kuchelewa kutoka kwa albam hiyo ni kutokana na kutokamilika kwa collabo na wasanii wengine wa nje ya Tanzania.

 Ameendelea kusema kuwa “Albam nitatoa mwakani, ilikuwa tuachie mwaka huu lakini kwasababu ya ukubwa wa mastering kwa Harmy B na pia tunaitaji kupata collabo kubwa.

Mkali huyo aliongeza kuwa wako kwenye mpango kuwashirikisha kwenye albam hiyo Khaligraph Jones na Nyanshiski wote kutoka Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *