Akiongea na mwandishi wa habari akiwa kwenye ndege kuelekea Greensboro North Carolina, Bi Clinton amesema anajiskia vizuri baada ya mapumziko ya siku tatu.
Mpinzani wake wa Chama cha Republican, Donald Trump ametoa barua kutoka kwa daktari wake ikionesha kuwa ana afya njema.
Barua hiyo inaonesha kuwa anatumia dawa ili kupunguza unene na kiwango kilichopitiliza cha uzito, lakini hatumii kilevi wala kuvuta sigara.
Uchaguzi wa Marekani utafanyika mwezi Novemba ambapo kampeni zake zimekuwa na vuta ni kuvute kutoka vyama vikubwa viwili vya Democratic na Republican.