Mwanamziki nyota wa Marekani, Ciara amesema kuwa anajisikia faraja kwenye maisha yake mapya ya ndoa na mume wake mwanamichezo, Russel Willson jinsi wanavyoishi.

Ciara amesema hayo wakati wa mahojiano na jarida la Harper Bazaar na kusema kuwa furaja yake imeongeza baada ya kuolewa na mwanaume huyo kwani tofauti na mpenzi wake aliyepita namna wanavyoishi.

Mwanamuziki huyo ambaye anatarajia kupata mtoto wake pili kutokana ujauzito alionao kutoka kwa mpenzi wake huyo.

Pia Ciara ameelezea jinsi mtoto wake anayeitwa ‘Baby Future’ aliyezaa naye rapa Future kwa kusema anajisiki raha kumuona mwanawe akiwa na furaha muda wote.

Amesema “Kumuona mwanangu anakimbia kimbia kila kona ya nyumba inanipa faraja kubwa sana na very soon watakuwa wawili wakikimbizana mle ndani! Maisha yetu yatakuwa kukimbizana mwanzo mwisho.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *