Muigizaji wa Bongo Movie, Chuchu Hans amefunguka kuwa watu wanaomhukumu kuwa anakosea kuwa karibu na mpenzi wake Vincent Kigosi ‘Ray’ wakati huu wa mfungo wa Ramadhani na yeye ni Muislamu waache kwani wao siyo Mungu.

Chuchu amesema kuwa kuishi na mzazi mwenziye huyo kwa ajili ya kazi haoni kama ni dhambi lakini anashangaa watu wanavyotoa hukumu mitandaoni kwamba anakosea.

“Mimi ninachojua wa kumhukumu mtu ni Mungu pekee kwa sababu yeye ndiyo anajua ukweli wote na anajua kila kitu cha binadamu na si mtu mwingine, najua nilivyo huku na Ray watu wanasema sana tu lakini sijali,”.

Muigizaji huyo amebaahatika kupata mtoto mmoja wa kiume Ray ambaye pia ni muigizaji wa Bongo Movie.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *