Muigizaji wa Bongo Movie, Chuchu Hans amedai kwamba usaliti aliofanyiwa mpenzi wake Ray Kigosi umemuumiza sana mpaka ameamua kuachia filamu inayohusu mkasa huo.
Chuchu ametoa tuhuma hizo wakati akizindua tamthilia yake mpya iitwayo “Play Boy” ambayo itakuwa ikirushwa kupitia application ya SwahiliFlix.
“Tamthilia hii ni mjumuisho wa matukio ya kweli yaliyowatokea watu wangu wa karibu pamoja na mimi mwenyewe, na inahusu mwanaume ambaye anakuwa kwenye mapenzi na wanawake zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.” ameeleza.
Chuchu anadai tamthilia hiyo ambayo pia imesheheni mastaa kibao wa maigizo wa zamani kama vile Waridi, Kelvin wa Kaole, Single Mtambalike Richie.
“Nimepata hamsa zaidi ya kuiachia wakati huu baada ya kusalitiwa, napitia maumivu ya mapenzi”amesema mwigizaji huyo.