Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Cameroon, Christian Bassogog amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyomalizika nchini Gabon mwaka huu 2017.

Mchezaji huyo amekuwa msaada mkubwa kwa timu yake ya Cameroon kuweza kutwaa Kombe la Afcon baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Misri na kutajwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashindano na Kamati ya Ufundi ya CAF na kikundi cha Watathmini.

Orodha ya wachezaji wengine waliofanya vizuri katika michuano hiyo ni Mchezaji Bora wa Benjamin MOUKANDJO (Cameroon), Tuzo ya Fair Play – Misri, Mfungaji Bora-Junior KABANANGA (DRC) Mabao 3, Kikosi cha Mashindano cha CAF – Kipa Fabrice ONDOA (Cameroon),Mabeki- Modou Kara MBODJI (Senegal), Ahmed HEGAZY (Misri), Michael NGADEU (Cameroon)

Viungo-Charles KABORE (Burkina Faso), Daniel AMARTEY (Ghana), Bertrand TRAORE (Burkina Faso), Christian ATSU (Ghana), Mohamed SALAH (Misri) .

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *