China imezindua manowari yake ya kwanza yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita yenye uzani wa tani 50,000.
Hatua hiyo inachukuliwa kama ishara ya karibuni zaidi ya kujiimarisha kwa taifa hilo katika nguvu za jeshi lake la majini.
Vyombo vya habari nchini China vinasema meli hiyo, ambayo inawezesha ndege kuruka na kutua juu yake, ilisafirishwa kutoka eneo ambalo ilikuwa ikiundiwa Dalian na kuwekwa baharini.
Meli pekee kubwa ya kubeba ndege inayomilikiwa na China ni meli ya Liaonong, ambayo ni meli ya enzi za muungano wa Usovieti iliyofanyiwa ukarabati.
Meli hiyo inatarajiwa kuanza kazi rasmi mwaka 2020 baada ya kukamilika katika kila idara kwenye meli hiyo.