Staa wa hip hop, Chid Benz na wenzake watano jana wamepandishwa katika mahakama ya Wilaya ya Ilala huku upande wa Jamhuri ikiiomba mahakama kuwaweka chini ya usimamizi maalum kwa kipindi cha miaka mitatu.

Polisi wa kituo cha Msimbazi waliwasilisha kiapo na kuiomba mahakama kuamuru wawekwe chini ya uangalizi maalum ikiwa ni pamoja na kusaini bondi na kuwa na wadhamini, ili kuhakikisha hawajihusishi tena na matumizi ya dawa za kulevya.

Mahakama iliridhia maombi hayo na kuamuru msanii huyo na wenzake kuhakikisha wanaripoti katika kituo cha polisi cha Msimbazi mara moja kila mwezi kwa kipindi cha miaka miwili.

Aidha, kila mmoja alitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao walitakiwa kusaini bondi ya shilingi milioni mbili kila mmoja.

Chid Benzi aliwahi kupandishwa kizimbani baada ya kukamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) miaka miwili mitatu iliyopita akiwa na kiasi kidogo cha dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati.

Msanii huyo alikiri kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na amewahi kuhudhuria matibabu katika jumba maalum (rehab) kwa ajili ya matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *