Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Rashid Makwiro maarufu ‘Chid Benz’ amesema kuwa amechoshwa na watu wanaomkebei kuhusiana na kukonda kwake na kuwataka wafatilie maisha yao.

Kauli ya mwanamuziki huyo inakuja kufuatia baadhi ya mashabiki kumkebei kwake kutokana na kukonda kwake baada ya matumizi ya madawa ya kulevya.

Chid Benz amesema kauli za watu wa mitandao zimekuwa zikimuandama juu hali yake kiafya ikiwa pamoja na Kukonda kwake huku wengi wakimshtumu kutumia madawa ya kulevya bila kujua kwamba hali ya hewa ndio iliyomfanya apungue.

Kuhusiana na tuhuma anazotupiwa na mashabiki mitandaoni kuwa anatafuta kiki ya kurudi kimuziki chibenz amewaonya mashabiki wanaomfatilia mitandaoni kuacha tabia hiyo.

Chid Benz amemshutumu msanii wa Bongofleva Jux kwa madai ya kutomlipa pesa zake katika ya show ya Money & Love iliyoandaliwa na Jux pamoja na Vanessa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *