Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Chemical ameweka wazi kuwa yeye siyo muumini wa kutumia kinga ndiyo maana mara nyingi anapenda kuwa kwenye mahusiano na mtu ambaye ni muaminifu.
Amesema kuwa “Mara ya mwisho kutumia kinga wakati nafanya mapenzi ni muda kidogo, ila kiukweli mimi sio shabiki wa kinga kabisa.
Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa mambo ya kinga kwa upande wake hapana ndiyo maana anapenda sana kuwa na mtu aliyetulia.
Msanii huyo ameweka wazi kwa sasa hayupo kwenye mahusiano na mtu yoyote kwa kuwa ameamua kuchagua kutengeneza maisha yake na kuhofia kuumizwa moyo wake.
Mwanamuziki huyo ni miongoni mwa wasaniii wa kike wanaoendelea kufanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva.