Jukwaa la wachekeshaji wa majukwaani, Cheka Tu kusaka vipaji mikoa mitano huku mshindi kulamba milioni kumi.

Hayo yamebainishwa na  kiongozi wa kundi hilo, Coy Mzungu  katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu shindano hilo.

Mzungu amesema mashindano hayo yanatarajia kufanyika mikoa mitano ya Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma na Dar es Salaam ambapo mshindi wa kwanza atapata zawadi ya Sh10 milioni.

Mbali na fedha, washindi hao watazawadiwa viwanja wilayani Bagamoyo na kupewa ajira za moja kwa moja Cheka Tu.

Amesema lengo la kuazisha mashindano hayo ni kuzalisha vipaji vya fani ya uchekeshaji na kuinua vijana wenye uwezo.

Kwa upande wao majaji akiwemo Zembwela, amesema hawategemei kuona wachekeshaji wake hususani wanaume wakienda wamevaa magauni, au kupaka makeup ili wafanane kama wanawake.

Wakati mchekeshaji Clayton Chipando maarufu kwa jina la Baba Levo, yeye amewashauri vijana kuchangamkia fursa hiyo, kwani mbali ya kupata ajira kama unatoka mkoani kwa Sh10 milioni kumi unapata hela ya kuanza kujenga nyumba kwa kiwanja atakachopewa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa vipindi vya Wasafi, Jamal Mustapha amesema angependakuona wanawake wakijitokeza kwa wingi katika kinyang’anyiro hicho ili kuongeza idadi ya wachekeshaji wa kike ambao kwa sasa ni wachache.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *