Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Chege amefunguka tetesi zilizodaiwa kuwa yeye na Diamond walipishana kisa Mbosso kusainiwa WCB.

Chege amesema kuwa ‘Nilisikia Mbosso kusainiwa WCB wala sikupewa taarifa yoyote kutoka kwa kiongozi wangu wala kutoka kwa kiongozi wa Yamoto Band, sio suala baya,  Je huku umeondoka vizuri ama umeondoka vibaya mbona kimya sina taarifa’– Chege

Pia amesema kuwa ‘Sikumlaumu Diamond alivyoongea Radioni kwasababu sikuulizwa na kama ningeulizwa basi ningefanunua kauli yangu niliyoitoa na wala sikuwa na sababu kumtakia mabaya Mbosso kwani ndie msanii pekee ambae nilikuwa nampenda Yamoto Band’.

Ameendelea kusema ‘Mbosso nimekutana nae Dodoma na nimeongea nae Mengi sana na nikamwambia kauli yangu ilieleweka vibaya na nimemtakia kila la heri WCB kwenye kazi zake na wala sina chuki yoyote’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *