Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtaka mgombea udiwani katika kata ya Buhangaza wilayani Muleba kujiondo kwenye kinyang’anyiro hicho cha uchaguzi.

Maamuzi hayo yanakuja kufuatia kutekwa kwa mgombea huyo na watu wasiojulikana kwa zaidi ya siku mbili.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa chama hicho,  Dtk. Vincent Mashinji huku akisema jeshi la polisi linatakiwa kufanya uchunguzi wa haraka ili  kubaini waliomteka mgombea huyo wa udiwani.

Mashinji amesema kuwa Makoti alitekwa Februari 2 mwaka huu katika mazingira ya kutatanisha na  kupatikana Februari 5 akiwa ametelekezwa  eneo la  Hospitali ya Kagando  iliyoko Muleba ambako mpaka sasa ndipo amelazwa.

 Pia amesema kuwa watekaji walimteremsha katika bodaboda aliyokuwa amepanda wakati akitokea kwenye  mchakato wa kampeni za udiwani ambapo watekaji hao walikuwa ndani ya gari aina ya Toyota RAV 4.

 Ameongeza kuwa Makoti alitakiwa kukukubali kupokea pesa ambazo walikuwa nazo  ili  aweze kujitoa katika kinyang’anyiro hicho cha udiwani  lakini baada ya kukataa ndipo alianza kusulubiwa hadi hapo walipotimiza azima yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *