Aleksander Ceferin amechaguliwa kuwa rais mpya wa shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) baada ya kumshinda mpinzani wake Michael van Praag kwenye uchaguzi uliofanyika jana.

Rais huyo anachukua nafasi ya aliyekuwa rais wa shirikishi hilo Michel Platini aliyejiuzuru kutokana na kashfa ya ubadhirifu wa fedha wakati akiwa kiongozi wa chombo hiko cha mpira barani Ulaya.

Baada ya kuchaguliwa kiongozi huyo aliwashukuru wajumbe waliompigia kura kwenye uchaguzi huo na kusema kwamba atashirikiana nao kuhakikisha soka la Ulaya linasonga mbele kabisa kipindi cha uongozi wake.

Platin: Rais wa zamani wa UEFA.
Platin: Rais wa zamani wa UEFA.

Pia Coferin amesema kuwa anaunga mkono pendekezo la nchi zenye ligi bora ziingize timu nne moja kwa moja kwenye makundi ya ligi ya mabingwa tofauti na sasa ambapo timu iliyoshika nafasi ya nne inaanza kucheza mechi za mchujo.

Kauli hiyo la rais huyo mpya inakuja kufuata UEFA na klabu za Ulaya kukubaliana mabadiliko kwenye ligi ya mabingwa mwezi uliopita wa kuingiza timu nne kwenye hatua ya makundi.

Ceferin kabla ya kuchaguliwa kuwa rais wa UEFA alikuwa kiongozi wa shirikisho la soka nchini Slovenia toka mwaka 2011 na sasa amekuwa rais wa UEFA mpaka mwaka 2019

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *