Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamphrey Polepole amesema kuwa Chama hicho kinasikitishwa na muendelezo wa matukio kwenye eneo la Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani.

Polepole amesema kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipofanya mkutano na waaandishi wa Habari kuhusu hali ya amani nchini pamoja na masuala mengine ya kimaendeleo.

Amesema kuwa wamelifatilia suala hilo na kuona ni vyema kusimama na Watanzania wakiwemo Wanachama wa CCM katika maeneo hayo na kusema kuwa wapo pamoja na wanatambua wanapitia wakati mgumu.

 Pia ameongeza kwa kusema kuwa ‘Sitaki kusema maneno makubwa kwamba zaidi kwamba ikiendelea tutapenda kuona watu wengine wanawajibishwa.. niseme pia tumesikitishwa sana, sisi tunaamini demokrasia ya vyama vingi ni mshikamano lakini tunahisi kama tumeachwa wenyewe, tumevunjika moyo sana, ukimya wa wenzetu vyama vingine vya siasa umetusikitisha.

Kwa upande mwingine Polepole amewataka wananchi kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake anazofanya katika Serikali ya awamu ya Tano.

Polepole amepongeza suala la Rais Magufuli kuhusu uchunguzi wa mchanga wa dhahabu katika makontena yaliyopo katika bandari nchini ambapo lipoti ya uchunguzi huo imekabidhiwa jana kwa Rais  Magufuli.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *